Traktate
Prof. Dr. Werner Gitt
Suaheli: Wie komme ich in den Himmel?
Nitawezaje kuingia Mbinguni?
Die grundlegende Frage, die suchende Menschen sich stellen, wird hier von Prof. Dr. Werner Gitt beantwortet. "Wie findet man den Himmel?" Auf jeden Fall nicht durch eigene Anstrengungen oder Konzepte. "Was aber bringt uns wirklich in den Himmel?" Gott hat die Einladungen für den Himmel schon verteilt wie im Gleichnis des Menschen, der zu einem großen Fest Einladungen verschickte. Doch viele Menschen redeten sich heraus.
Prof. Dr. Gitt ruft dazu auf, nicht so "kurzsichtig" wie diese Leute zu sein. Jesus will uns vor der Hölle erretten und diese wird kein Vergleich zu der sogenannten "Hölle von Auschwitz" sein. Er hat am Kreuz für unsere Schuld bezahlt, wir müssen diese Einladung nur annehmen, dann ist ein Platz im Himmel "gebucht". Ein Entscheidungsgebet soll den Lesern dabei helfen.
Dieses Traktat eignet sich besonders gut zur Weitergabe an suchende Menschen!
8 Seiten, Best.-Nr. 120-52, Kosten- und Verteilhinweise | Eindruck einer Kontaktadresse
Nitawezaje kuingia Mbinguni?
Watu wengi hulikwepa swali la milele. Twaona hayo hata kwa wale ambao hufikiria hatima yao. Mwigizaji msanifu wa filamu wa kimarekani Drew Barrymoore (kuz. 1975) amemwigiza mtoto katika filamu ya »E.T.«. Alipofikia umri wa miaka ishirininanane akatamka: »Iwapo nitafariki kabla ya paka wangu, alishwe jivu la maiti yangu. Ndivyo nitakavyoendelea kuishi ndani ya paka wangu.« Je, hali hii ya kutoelewa na mtazamo mfupi kwa mauti haisikitishi?
Wakati wa Yesu watu wengi wakamjia. Mara nyingi mahitaji yao yalikuwa ya kudunia:
- Wenye ukoma kumi walitaka kupona (Luka 17:13),
- Vipofu walitaka kuona tena (Mathayo 9:27),
- Mtu fulani alitaka kusaidiwa kwa ugomvi wa uridhi (Luka 12:13-14),
- Mafarisayo wakaja na swali la mtego, kama ni halali kulipa kodi kwa Kaisari (Mathayo 22:17).
Watu wachache tu wakaja kwa Yesu, ili wafundishwe jinsi ya kuingia Mbinguni. Kiongozi kijana tajiri akamjia na swali: »Mwalimu mwema, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa milele?« (Luka 18:18). Akaambiwa afanye nini: auze yote ambayo moyo wake umeyashika na kumfuata Yesu. Sababu alikuwa tajiri sana, hakulifanyia kazi shauri hilo na kukosa kuja mbinguni. Watu wengine hawakuitafuta mbingu, lakini wakaongozwa kule walipokutana na Yesu. Wakaishika mbingu mara tu. Zakayo akatamani kumwona Yesu. Amepata zaidi kuliko alivyotegemea. Nyumbani kwake Zakayo, wakati Yesu alipomtembelea, walipokunywa chai, akaiona mbingu. Yesu akatamka: »Leo wokovu umefika nyumbani humu« (Luka 19:9).
Twaigunduaje mbingu?
Baada ya hayo tuliyoona hapo juu twaweza kusema:
- Ufalme wa mbinguni twaupokea siku maalum. Ni vema kuyajua hayo, sababu hata wewe msomaji mpendwa, utaweza kushika uzima wa milele kwa Mungu leo.
- Hatujipatii ufalme wa mbinguni kwa jitihada maalum.
- Ufalme wa mbinguni waweza kuugundua ghafla na bila maandalizi.
Mipango yetu ya kutufikisha mbinguni ni batili, tusipoyafuata maneno ya Mungu. Mwimbaji fulani akatunga katika wimbo habari ya mchekeshaji aliyestaafu kazi yake katika „sarakasi“: »Bila shaka atafika mbinguni kwa sababu aliwafurahisha watu.« Mfadhili wa kike akajenga nyumba kwa maskini, ambamo wanawake 20 waliweza kuishi bure. Akawapa sharti moja tu: Watoe ahadi kuuombea wokovu wa roho yake kila siku kwa muda wa saa moja.
Je, nini inatupeleka kweli mbinguni?
Ili ajibu swali hilo wazi na sawa, Yesu akasimulia mfano. Katika Injili ya Luka, sura ya 14:16 akaeleza habari ya mtu [ktk. mfano badala ya Mungu], aliyeandaa sherehe kubwa [ktk. mfano kwa Mbingu] na kuwapelekea mialiko watu maalum tu. Majibu yao yanasikitisha. Mmoja baada ya mwingine hutoa udhuru. Wa kwanza hueleza: »Nimenunua shamba...«, wa pili: »Nimenunua ng´ombe jozi tano wa kulima...«, wa tatu: »Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.« Yesu akamaliza mfano wake na maamuzi yake aliyetoa mialiko: »Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu« (Luka 14:24).
Hapo waona wazi, twaweza kuupata au kuupoteza mbingu. Sharti, kuyapokea au kuyakataa makaribisho. Je, yaweza kurahisishwa zaidi? Haiwezekani! Watu wengi hawatakataliwa mbinguni kwa sababu hawakuijua njia, bali kwa sababu wameyakataa mwaliko.
Hawa watu watatu wa mfano tusiwaige, kwa sababu hawataishiriki sherehe ile! Kwani sherehe haitafanyika? Hasha! Baada ya kupata udhuru zao, mwenye sherehe hutuma mialiko mingine kotekote. Hamna tena kadi za mwaliko zenye marembo ya dhahabu. Sasa ni mbiu tu: »Njooni!« Na kila anayekubali kuja, hakika atapata nafasi yake kwenye sherehe. Yatokea nini sasa? Ndiyo, watu wanakuja – tena kwa wingi. Baada ya muda mwenye sherehe akaipima nafasi tena: Kumbe, nafasi ipo bado, viti vipo! Huwaambia watumishi wake: »Nendeni tena! Mkawakaribishe na wengine zaidi!«
Hapo nataka kutufananisha sisi na mfano huo, sababu unaeleza hali yetu ya leo. Mbinguni kuna nafasi kwetu bado na Mungu akuambia: »Njoo, upange kiti chako mbinguni! Uwe na hekima na jiwekezee kwa milele! Amua leo!«
Mbingu ni nzuri isivyoelezeka na kwa hiyo Bwana Yesu ameifananisha mbingu na sherehe. Twasoma hivi katika 1Korintho (Sura 2:9): »Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.« Hakuna hali, kwa kweli hamna kabisa duniani, inayofanana na mbingu. Uzuri wake hauelezeki! Tusiikose mbingu kwa vyovyote vile, sababu ni wa thamani mno. Mmoja ametufungulia mlango wa kuingia mbinguni. Huyu ni Yesu, mwana wa Mungu! Ni kwa ajili yake tu na ni jambo la kumshukuru, ya kwamba ni rahisi sasa kwetu kufikia kule. Twahitaji kuchukua uamuzi tu. Asiyefuata mwaliko huo haoni mbali, kama hawa watu katika mfano.
Ukombozi huja kwa Bwana Yesu
Katika Matendo ya Mitume (Sura 2:21) twasoma mstari muhimu sana: »Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana [= Yesu] ataokolewa.« Ni mstari muhimu wa Agano Jipya. Paulo alipokuwa gerezani Filipi, akamwambia Mkuu wa gereza: »Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako« (Matendo 16:31). Ingawa habari hii ni ya kifupi, yagusa na kubadilisha maisha. Usiku ule Mkuu wa gereza akakata shauri na kumgeukia Yesu.
Jambo moja lazima tujue: Yesu anataka kututoa kutoka katika njia inayoelekea upotevuni na jahanamu. Biblia hueleza kuhusu mbingu na jahanamu ya kwamba watu watakuwa huku kwa milele. Mahali pamoja ni pazuri sana na pengine ni pa kutisha sana. Hapana mahali pa tatu. Hakuna mtu atakayesema dakika tano baada ya kufa kwake, kifo ndicho mwisho wa yote. Bwana Yesu ndiye mwamuzi wa yote. Tutakapokuwa milele ni uamuzi wa mtu mmoja tu: Yesu – na uhusiano wetu pamoja naye!
Nilipokuwa Poland kwa ziara ya mafundisho, tukatembelea pia „Kambi la maangamizo” ya Auschwitz. Gereza lile la „Maangamizo“ (CC) liliwekwa na “Wanazi” wakati wa Vita vya pili vya Ulimwengu huko Polandi Kusini. Kule Auschwitz wakateketezwa kimpango watu waliotafutwa na „Wanazi“ (Chama tawala cha kijerumani wakati ule). Mambo mabaya na ya kinyama yametendeka pale. Wakati wa mwaka 1942 bis 1944 watu zaidi ya milioni 1.6 na hasa wayahudi wameuawa kwa gesi ya sumu na hatimaye kuchomwa moto. Kihistoria wakati ule umefahamika kuwa »Jahanamu ya Auschwitz«. Nimelitafakari neno hilo, tulipoongozwa na mtu pale katika chumba kimoja, walipouwawa kila mara mojamoja kundi la watu 600. Ni vibaya sana visivyoelezeka. Lakini je, kweli hii ni jahanamu?
Tuliweza tembelea na kujionea mahali pale, sababu tangu 1944 ule ukatili mkuu umekoma. Mahali pale panaweza kutembelewa sasa na kila mtu, bila hofu ya kuteswa au kuuwawa. Vile vyumba vya gesi vya Auschwitz vilikuwa ni vya muda. Lakini Jahanamu katika Biblia ni ya milele.
Katika ukumbi wa mapokezi siku hizi kule, nikaona picha ambayo yaonyesha ule mwili wa Kristo msalabani. Mfungwa mmoja alikuwa ameparura na msumari matumaini yake ukutani. Hata huyu msanii akafa pale. Lakini alimfahamu Mwokozi Yesu. Akafa mahali pa kutisha sana, lakini mbingu ikafunguliwa kwake. Lakini kutoka katika Jahanamu ile, ambayo Bwana Yesu anatuonya katika Agano Jipya (k.mf. Mathayo 7:13; 5:29-30; 18:8), hamna mlango wa kutokea wala ukombozi wa mtu aliyekwishafika kule. Kwa sababu jahanamu, tofauti na Auschwitz inafanya kazi daima na haiwezi kamwe kutembelewa wala kuangaliwa.
Hata mbingu ni ya milele. Ndipo mahali ambapo Mungu hutaka kutufikisha. Mukubali mwaliko wa kufika mbinguni. Mliitie jina la Bwana Yesu na kufanya „booking“ ya nafasi mbinguni! Mwanamke fulani akaniuliza, baada ya hotuba yangu: »Je, yawezekana kufanya „booking“ mbinguni? Yasikika kama ofisi ya wakala wa usafiri!« Nikamwitikia: »Asiyekata tiketi, hafiki anapokusudia. Mkitaka kufika Hawaii, mnahitaji tiketi hai ya ndege.« Akauliza zaidi: »Tiketi ya ndege lazima ilipwe?!« – »Ndiyo, tiketi ya mbinguni vilevile! Lakini ni ghali sana na hakuna mtu awezaye kuilipa. Ni kwa sababu ya dhambi zetu. Mungu hawezi kuivumilia dhambi katika mbingu yake. Anayetaka, baada ya maisha yake, kuishi milele na Mungu mbinguni, anahitaji kuwekwa huru na dhambi yake kwanza. Ukombozi huo ameleta mtu aliyekuwa bila dhambi – na huyu mtu ni Yesu Kristo. Yeye peke yake aweza kulipa! Isitoshe, ameshalipa na damu yake, kwa kifo chake cha msalabani.«
Je, mimi nifanyeje ili nifike mbinguni? Mungu atuletea mwaliko wake wa kupokea wokovu. Mistari mingi ya Biblia yasisitiza mwaliko huo, ili tuitikie wito wa Mungu:
- »Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba!« (Luka 13:24).
- »Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia!« (Mathayo 4:17).
- »Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.« (Mathayo 7:13-14).
- »Shika uzima ule wa milele ulioitiwa« (1Timotheo 6:12).
- »Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako« (Matendo 16:31).
Mialiko hiyo yote yastusha sana na kuamusha. Twajisikia ya kwamba ni ya muhimu sana, pia yatuhamasisha kweli. Kwa maana hiyo basi, tuitikie mwaliko huo wa kuja mbinguni kwa sala yetu kama ifuatavyo:
»Bwana Yesu Kristo, nimeishi hadi leo kama wewe haupo. Nimetambua sasa, wewe u nani na kwa sababu hiyo naja kwako mara ya kwanza kwa sala. Najua sasa ya kwamba kuna Mbingu na Jahanamu. Niokoe na jahanamu, mahali ambapo kwa dhambi yangu na kutoamini kwangu ningestahili kwenda. Ni hamu yangu, kuwa pamoja nawe mbinguni milele. Najua ya kwamba siwezi kufika mbinguni kwa matendo yangu mazuri, bali kwa kukuamini wewe. Kwa sababu wewe hunipenda ukanifia msalabani na kubeba makosa yangu yote na kunilipia. Nakushukuru kwa hayo. Waona dhambi zangu, hata yale yote kuanzia ujana wangu. Kila dhambi mojamoja ya maisha yangu waijua – yote ninayokumbuka na zile ambazo nalisahau. Wewe wanijua kabisa. Waelewa hisia zote za moyo wangu, ikiwa ni furaha au masikitiko, ustawi au kukata tamaa. Mimi ni kama kitabu kilicho wazi mbele yako. Jinsi nilivyo na jinsi maisha yangu yalivyo hadi sasa, siwezi kuishi nawe na Mungu aliye hai na ningestahili kuikosa mbingu. Kwa hiyo nakusihi, unisamehe dhambi zangu zote. Nasikitika kwa ajili ya dhambi zangu. Tafadhali, nisaidie kuvua yote yasiyo sawa mbele zako na unipatie uadilifu unaoniwezesha kuishi chini ya baraka zako. Nifungulie uelewo wa Neno lako la Biblia. Nisaidie kuelewa unachotaka kuniambia, ili nipate nguvu mpya na furaha ya maisha kutoka katika Neno lako. Wewe ni BWANA wangu kuanzia sasa. Mimi ni mali yako na ninataka kukufuata. Unionyeshe njia ambayo naweza kwenda. Nakushukuru kwamba umenisikia. Naamini ahadi yako ya kwamba kwa kukugeukia nimepata kuwa mtoto wa Mungu, ambaye atakuwa pamoja nawe mbinguni milele. Nafurahi sana kujua, mimi ni pamoja nawe na wewe u kwa kila hali upande wangu. Nisaidie kukutana na watu wanaokuamini na niweze kushiriki katika kanisa ambapo naweza kupata kusikia na kulishwa Neno lako daima. Amina.«
Mkurugenzi na Profesa mstaafu
Daktari-Injinia Werner Gitt